Lyrics to "nani" by Susan Of Gogo Simo

  nani by Susan of Gogo Simo

najua ni wengi wanataka tutengane,
wataka tuwe mbali mbali, haitowezekana
haitokuwa, wajaribu kwengine.
sababu hakuna, cha maana hawana.
ya nini tuwe mbali mbali,
dhamira yao nini, watamenya wapi ili watufikie

chorus x2
ndio maana mi nasema,
nani atakaye jaribu,
kupitia njia ile,
nimpe mkono.

verse 2
penzi ni letu, si tulipokutana
hakuna ambaye alikuweko
ya nini mjitie, mjisumbue akili, na njia ni nyingi.
si mtafute wenu mzuri kama wangu,
ya nini tutiane khere, si kwamba si tambui, naelewa kila kitu,
mwanionea wivu.

chorus x2

bridge

(anipenda nampenda) x2
nishazama

sibanduki, habanduki
mtapanda mkishuka
tu imara

milele, na milele

*instrumental

chorus x4




"toka leo" lyrics by Susan of Gogo Simo

toka leo lyrics:

intro

uwe wangu x3

repeat set

verse 1

nimekuwa nikikutazama toka mbali kwa muda sasa
nikaamua uwe wangu wa ndani
sasa nitakueleza, sitoweza kuya weka ndani tena
nimejaliwa, ukaniona, haki huto niponyoka
nitahakikisha

chorus:
na toka leo
uwe mi wangu milele
na toka leo x2

verse 2:

nimekuwa nikitamka jina lako kwa muda sasa
huja wakati ukanijia ndotoni
sasa nimekueleza, ni raha kwangu
kujua wanipenda, nimejaliwa, ukaniona
haki nakupenda, na kesho tena

chorus x4

bridge

mahabuba nikupe langu penzi
mahabuba unipe lako penzi

chorus x4

na toka leo
uwe mi wangu milele
na toka leo x2